Balozi wa Maji, Mhandisi Mrisho Mpoto akiwa pamoja na viongozi wa Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Rukwa na wananchi alipotembelea chanzo cha Maji cha Nzovwe 1 kilichopo jijini Mbeya. Katika ziara hiyo, Balozi wa Maji alijionea ni namna gani ambavyo Bodi pamoja na wananchi wameweza kushirikiana kutunza chanzo cha maji ambacho mjini kati, amesema kuwa jambo hilo ni gumu sana, lakini Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Rukwa imefanikisha hilo. Ni jambo la kuigwa na mabonde mengine yote.